London,England.
Hatimaye Jack Wilshere jana ijumaa usiku alirejea uwanjani kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kuwa majeruhi na kukiongoza kikosi cha Arsenal cha U21kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya kikosi cha U21 cha Newcastle United.
Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Emirates Wilshere alicheza kwa dakika 65 akionekana mwenye kasi na ngangari kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Josh Da silva.
Mbali ya Wilshere,Thomas Rosicky nae alishuka dimbani hiyo jana na kucheza kwa dakika 45 huku akifanikiwa kupika bao la pili lililofungwa na Serge Gnabry.
Magoli ya Arsenal katika mchezo huyo yamefungwa na Dan Crowley 7, Mavidi 8 na Serge Gnabry 34 huku Krystian Bielik akijifunga dakika ya 24 na kuipa Newcastle United bao la kufutia machozi.
0 comments:
Post a Comment