Picha:Wachezaji wa FUS Rabat wakishangilia bao
Rabat,Morocco.
Sports Club Villa ya Uganda imeianza vibaya michuano ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF) baada ya jana ijumaa kuchapwa mabao 7-0 na FUS Rabat ya Morocco.
Katika mchezo huo ulichezwa huko Stade
Moulay Abdallah,Rabat,Mpaka mapumziko wenyeji FUS Rabat walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Mourad Batna 26,Ass Mandaw 34, Abdessalam Benjelloum 40.
Kipindi cha pili FUS Rabat iliongeza ushindi wake kwa mabao ya El Mehdi El Bassil 47, Marwane Saadane 70,Youssef El Gnaoui 81 na Fouzair dakika ya 90.
Timu hizo zitarudiana tena kati ya Aprili 19 au 20 huko Kampala Uganda na mshindi atakata tiketi ya kuingia hatua ya robo fainali.
0 comments:
Post a Comment