Genk,Ubelgiji.
Nyota ya mshambuliaji Mtanzania,Mbwana Samatta imeendelea kung'aa baada ya jana usiku kutokea benchi na kuifungia KRC Genk katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KV Oostende katika mchezo wa mtoano wa Ligi Kuu ya Ubelgiji uliopigwa huko Cristal Arena mbele ya watazamaji 16276.
Samatta alifunga bao hilo dakika ya 77, ikiwa ni dakika moja tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Mgiriki Nikolaos Karelis.
Mabao mengine ya KRC Genk yamefungwa na Alejandro Pozuelo dakika ya 12,Thomas Buffel dakika ya 21 na Neeskens Kebano dakika ya 85.
Ushindi huo unaifanya KRC Genk kufikisha pointi 27 katika nafasi ya 4 huku KV Oostende ikibaki na pointi 25 katika nafasi ya 5.
VIKOSI
KRC Genk : Bizot,
Castagne, Dewaest, Kabasele,Uronen, Ndidi, Pozuelo,Malinovskyi, Bailey, Buffel na Karelis.
KV Oostende :
Ovono, Lukaku, Siani, Berrier,Rozehnal, Jali, Pedersen,Jonckheere, Capon, Milic na Canesin.
0 comments:
Post a Comment