Manchester, England.
Manchester City imetoka nyuma na kuilaza West Bromwich Albion mabao 2-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliopigwa usiku wa leo katika dimba la Etihad.
Manchester City ambayo leo ilianza bila ya nyota wake watano wa kikosi cha kwanza ilijikuta nyuma baada ya Stephane Sessegnon kuifungia West Bromwich Albion bao dakika ya 6 akimalizia kazi nzuri ya James McCleash.
Dakika ya 19 Sergio Aguero aliifungia Manchester City bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Stephane Sessegnon kumwangusha Aleksandar
Kolarov katika eneo la hatari.
Samir Nasri aliifungia Manchester City bao la ushindi dakika ya 66 akimalizia pasi murua ya Kevin De Bruyne
VIKOSI
Manchester City: Hart; Zabaleta, Otamendi Mangala, Kolarov; Fernando, Delph, Navas,
Nasri; Bony, Aguero
Subs: Caballero, Demichelis, Clichy,Fernandinho, Toure, De Bruyne, Iheanacho
West Bromwich Albion: Foster; Chester, Evans,
McAuley, Dawson; Fletcher, Sandro; Berahino,McClean, Sessegnon; Rondon
Subs: Myhill; Olsson, Yacob, Gardner,Anichebe, McManaman, Leko
0 comments:
Post a Comment