Roma,Italia.
Kocha mkuu wa Leceister City Claudio Ranieri ametangazwa mshindi wa tuzo ya kocha bora wa mwaka wa Italia maarufu kama "Enzo Bearzot"
Ranieli,64 ameshinda tuzo hiyo kubwa baada ya kuiongoza Leceister City kutoka kunusurika kushuka daraja msimu uliopita mpaka kugombania ubingwa wa ligi kuu England.
Jana jumatano Rais wa chama cha soka cha Italia Carlo Tavecchio alimtangaza Ranieli kuwa mshindi huku akimuita kuwa ni Nembo ya Italia inayong'aa Ng'ambo.
Kabla ya kutua Leceister City Ranieri amewahi kuvifundisha vilabu vya Fiorentina,Valencia,
Atletico Madrid,Chelsea, Juventus,Roma,Inter Milan, Monaco na timu ya taifa ya Ugiriki.
Ranieli atakabidhiwa tuzo hiyo Mei 9 katika sherehe maalumu itakayofanyika huko Roma,Italia.
Washindi waliopita wa tuzo hiyo ni pamoja na Cesare Prandelli (2011), Walter Mazzarri (2012), Vincenzo Montella (2013), Carlo Ancelotti (2014) na Massimiliano Allegri (2015).
Tuzo ya Enzo Bearzot ilianza kutolewa mwaka 2011kama ishara ya kumuenzi kocha wa zamani Enzo Bearzot aliyeiwezesha Italia kutwaa kombe la dunia mwaka 1982.Bearzot alifariki mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment