London,Uingereza.
TAMU/CHUNGU!!Meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kuwauza nyota watatu wa klabu hiyo ili apate fedha za kumsajili Staa wa Juventus Mfaransa Paul Pogba katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.
Taarifa kutoka gazeti la The Daily Express zinasema kocha huyo Muitaliano jana jumanne alikutana na mabosi wa Chelsea kujadili masuala mbalimbali ya usajili wa majira yajayo ya kiangazi.
Moja kati ya Agenda kubwa katika kikao hicho imekuwa ni kumsajili Kiungo Paul Pogba mwenye thamani ya paundi milioni 80 na ili kutimiza azma hiyo Conte atawauza Oscar, John Obi Mikel na Willian
Wakati huohuo Conte ameripotiwa kuwa kabla ya msimu mpya atafanya mazungumzo na nyota wanne wa klabu hiyo Eden Hazard,Diego Costa,Nemanja Matic na John Terry kuhusiana na maisha yao ya baadae Stamford Blidge.
0 comments:
Post a Comment