728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 09, 2017

    Yanga yaelezea maandalizi yake kuelekea mchezo wake dhidi ya Zanaco Jumamosi


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Kikosi cha Yanga kimekamilisha maandalizi ya yake kuelekea katika mchezo wake wa Jumamosi hii dhidi ya Zanaco ya Zambia utakaochezwa kwenye Uwanja wa wa Taifa,jijini Dar Es Salaam.

    Akiongea na waandishi wa habari mchana wa leo kocha msaidizi wa Yanga Sc,Juma Mwambusi amesema "Maandalizi yote yamekamilika na tayari timu ipo kambini ikiendelea na mazoezi ya mwisho mwisho kwaajili ya kuikabili Zanaco kesho kutwa Jumamosi.


    "Tunaendelea vizuri na mazoezi yetu na tunamshukuru Mwenyenzi Mungu baadhi ya wachezaji wetu waliokuwa majeruhi ambao ni Donald Ngoma,Thabani Kamusoko na Amisi Tambwe tayari wamerejea na kuanza mazoezi na kikosi,kiujumla wachezaji wote wana umuhimu kwenye kikosi cha Yanga SC hivyo kwa yeyote ambaye atatumika kwa upande wetu ni sawa na hakuna tatizo."Alimaliza Mwambusi.

    Yanga itaumana na Zanaco Jumamosi hii katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora ya michuano ya klabu bingwa Afrika kabla ya kurudiana wiki mbili zijazo huko Lusaka,Zambia na timu itakayoshinda itaingia kwenye hatua ya makundi.

    Azam wao watacheza Jumapili Machi 12, mwaka huu na Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.  

    Waamuzi watakochezesha mchezo huo wanatoka Benin ambao ni Mwamuzi wa kati, Addissa Abdul Ligali na wasaidizi ni Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina huku Mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou na kamisha wa mchezo atakuwa Mohamed Omar Yusud wa Kenya.

    Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ni Sh 10,000 kwa VIP, Jukwa Kuu itakuwa ni Sh 5,000 na Mzunguko itakuwa ni Sh 3,000.

    Wakati huohuo, tiketi za waamuzi wa Tanzania walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto Louis 2000 ya Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo, wamepata tiketi zao za kusafiri.

    Katika mchezo huo ambao utafanyika ama Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati wasaidizi wake watakuwa ni Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Hery Sasii. Kamisha katika mchezo huo Na. 78 atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka Afrika Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga yaelezea maandalizi yake kuelekea mchezo wake dhidi ya Zanaco Jumamosi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top