Paris,Ufaransa.
KIUNGO wa Psg,Thiago Motta (Pichani) huenda akaingia matatati baada ya kumjeruhi shabiki mmoja wa klabu kwa kumgonga kwa gari alfajiri ya leo.
Motta,34,ambaye hakuichezea Psg kwenye mchezo wa jana Jumatano wa ligi ya mabingwa Ulaya ulioisha kwa mabingwa hao wa Ufaransa kuchapwa mabao 6-1na Barcelona, amekutwa na mkasa huo kwenye uwanja wa ndege wa Le Bourget muda mfupi baada ya kikosi cha Psg kurejea nyumbani kikitokea Barcelona.
Imeripotiwa kuwa mashabiki wenye hasira zaidi ya arobaini waliokuwa uwanjani hapo walianza kufanya fujo na kuporomosha matusi mazito mara baada ya kuwaona wachezaji wa Psg wakitoka ndani ya uwanja huo.
Kama hiyo haitoshi mashabiki hao walifikia mpaka hatua ya kuanza kuparamia magari ya wachezaji hao na ndipo shabiki mmoja alipojikuta akikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari aina ya Porsche iliyokuwa ikiendeshwa na Motta huku ndani akiwepo pia mke wake, Francisca
Bado haijafahamika kama Motta alimgonga shabiki huyo kwa makusudi ama ilikuwa ni bahati mbaya.
0 comments:
Post a Comment