Lubumbashi,DR Congo.
MABINGWA wa DR Congo na mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho barani Afrika,TP Mazembe wameendelea kuonyesha kuwa kwao pesa siyo tatizo kabisa hii ni baada ya jana Alhamis kumsajili beki wa kulia wa Ubelgiji,Anthony Vanden Borre kwa mkataba ambao haujawekwa wazi kuwa ni wa muda gani.
Vanden Borre mwenye umri wa miaka 29,aliyeanzia soka lake kwenye kikosi cha watoto cha Anderlecht kilichokuwa na wakali kama Vincent Kompany atakuwa akivalia jezi namba 68 katika kipindi chote atakachokuwa na timu hiyo inayomilikiwa na bilionea,Moise Katumbi.
Vanden Borre alizaliwa mwaka 1987 huko Likasi,DR Congo kwa mama Mcongo na baba Mbelgiji.Alianza kukichezea kikosi cha wakubwa cha Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 16,mpaka sasa amefanikiwa kuichezea timu hiyo jumla ya michezo 28.
Astaafu,TP Mazembe yamrejesha uwanjani.
Januari 10,2017 Vanden Borre alitangaza kustaafu kucheza mpira.Mei 2,2017 TP Mazembe yatangaza kumsajili akiwa kama mchezaji huru.
Kabla ya kutua TP Mazembe,Vanden Borre aliwahi kukipiga katika vilabu vya Montpelier (Ufaransa),Anderlecht (Ubelgiji), Fiorentina (Italia), Genoa (Italia),Tavriya Simferopol (Ukraine) na Portsmouth (England).
Akipiga kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
Vanden Borre alikuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 23 kilichoiwakilisha Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia ziliyofanyika nchini Brazil mwaka 2014 ambapo alicheza mchezo mmoja peke yake.Korea Kusini.
0 comments:
Post a Comment