Gent,Ubelgiji.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta (Pichani) amefunga mabao mawili na kuipatia timu yake ya Genk ushindi wa mabao 5-2 ugenini dhidi ya Gent katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya 16 ya michuano ya Europa Ligi huko Ghelamco Arena.
Mpaka mapumziko Genk ilikuwa mbele kwa mabao 4-1 yaliyofungwa na Ruslan Malinovskiy 21', Omar Colley 33',Mbwana Samatta 41',Jere Uronen 45'.
Kipindi cha pili Samatta aliifungia Genk bao la tano katika dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa nahodha Thomas Buffel.Mabao ya Genk yamefunga na Samuel Kalu 27' pamoja na Kalifa Coulibaly 61' huku Jeremy Perbet akikosa mkwaju wa penati.
Timu hizo zitarudiana tena huko Luminus Arena wiki mbili zijazo na timu itakayopata ushindi mkubwa wa jumla itafuzu robo fainali.
0 comments:
Post a Comment