Munich,Ujerumani.
Bayern Munich imeendelea kuonyesha kuwa imekufa na imeoza kwa Muhispania Pep Guardiola baada ya kudaiwa kuandaa dau la £17m ili kuhakikisha kuwa kocha huyo wa zamani wa FC Barcelona aliyekaribia kumaliza mkataba anasaini mkataba mpya na kubaki Allianz Arena mpaka mwaka 2018.
Taarifa za uhakika toka katika gazeti la michezo la Munich liitwalo TZ limeripoti kuwa Bayern Munich imemuandalia kocha huyo mkataba wa miaka miwili ili kuzima mpango wa vilabu vya England ambavyo kwa kipindi kirefu vimekuwa vikiitaka huduma yake.
Ikiwa Guardiola atasaini mkataba huo mpya atakuwa akivuna £17m kwa mwaka na kuendelea kuwa kocha anayelipwa zaidi katika historia ya mchezo wa soka akiwaacha mbali makocha kama Arsene Wenger,Jose Mourinho,Louis Van Gaal na wengineo wengi.
0 comments:
Post a Comment