728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 11, 2015

    ARSENAL,MAN UNITED NA PSG ZAJIPANGA KUIBOMOA CHELSEA

    London,England.

    Vilabu vya Arsenal, Manchester United na Paris Saint Germain kwa pamoja vimeingia katika vita ya kuisaka saini ya kinda mwenye kipaji kikubwa cha soka Charly Musonda anayekipiga katika klabu ya Chelsea.

    Musonda,19 aliyesajiliwa na Chelsea mwaka 2012 akitokea Anderletch ya Ubelgiji amenukuliwa na gazeti la michezo la Ufaransa la Foot Mercato kuwa anataka kutimka Stamford Blidge baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza hali iliyovivutia vilabu vya Arsenal,Manchester United na Paris Saint Germain kuanza kumnyemelewa nyota huyo tegemeo la kikosi cha U21 cha Ubelgiji.

    Chelsea imeripotiwa kuwa itakuwa tayari kumuachia Musonda ikiwa dau la £10m inalolitaka litafikiwa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL,MAN UNITED NA PSG ZAJIPANGA KUIBOMOA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top