728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 11, 2015

    CHELSEA MBIONI KUMTIMUA ALIYEWASAJILI FALCAO,SALAH


    London,England.

    MKURUGENZI wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo yuko hatarini kutimuliwa kibarua hicho katika klabu hiyo baada ya kudaiwa kuvurunda katika madirisha yaliyopita ya usajili hali iliyofanya klabu hiyo iwe na msimu mbaya zaidi England.

    Habari za kuaminika zinadai Emenalo ameiingizia klabu ya Chelsea hasara ya £53m kwa kufanya usajili bomu.Baadhi ya wachezaji wanaodaiwa kusajiliwa na mkurugenzi huyo na kushindwa kuwika ni Filipe Luis,Papy Djilobodji, Mohamed Salah, Radamel Falcao na Juan Cuadrado.

    Pia Emenaro anashutumiwa kwa kujaza wachezaji na kisha kuwatoa kwa mikopo.Mpaka sasa Chelsea imetoa wachezaji 34 kwa mikopo kwenda vilabu mbalimbali vya ndani na nje ya England





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA MBIONI KUMTIMUA ALIYEWASAJILI FALCAO,SALAH Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top