728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 11, 2015

    JOSE MOURINHO AELEKEZA HASIRA ZAKE KWA LMA

    London,England.

    Kocha Jose Mourinho ameibuka na kukiponda chama cha makocha wa soka England (LMA) kwa madai kuwa chama hicho kimemtelekeza na kimeshindwa kumtetea wakati huu wa matatizo.

    Mourinho,52 amedai LMA imeshindwa kumtetea na imemuacha apambane vita ya peke yake na chama cha soka cha nchi hiyo FA.

    Mourinho ameongeza LMA imekuwa ikiwatetea makocha pindi wanapokuwa wamefukuzwa kazi lakini wanapokuwa katika matatizo ya kufungiwa au kupigwa faini kama anayokumbana nayo yeye huwa iko kimya.

    Mourinho amesema hayo zikiwa zimepita siku chache tu tangu akipwe marufuku ya
    kukanyaga uwanjani kuiongoza timu yake ilipokuwa ikivaana na Stoke City katika dimba la Brittania na kuambulia kichapo cha bao 1-0 baada ya FA kumkuta na hatia ya kutoa lugha chafu kwa mwamuzi.

    Mourinho ni kocha wa pili kulimwa adhabu ya kutokanyaga uwanjani wakati timu yake inacheza.Kocha wa kwanza kukumbwa na adhabu hiyo alikuwa ni Alan Pardew baada ya kumpiga kichwa kiungo wa Hull City David Meyler wakati huo akiifundisha Newcastle United.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JOSE MOURINHO AELEKEZA HASIRA ZAKE KWA LMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top