728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, November 12, 2015

    VIDAL,SANCHEZ URAFIKI KWISHA,WIVU WADAIWA KUWA CHANZO

    Santiago,Chile.

    Usione watu wanacheka,wanaongea ukadhani wanapendana kumbe mioyoni mwao wanachukia.Hii ndiyo hali halisi kwa nyota wa Chile Alexis Sanchez na Arturo Vidal.

    Kutoka gazeti la michezo la Chile la La Tercera nyota hao waliwahi kucheza pamoja katika klabu ya Colo Colo na wanaowakilishwa na wakala mmoja hivi sasa ni maadui wakubwa.

     La Tercera linazidi kuripoti kuwa chanzo cha uadui huo ni wivu ambapo kila nyota amekuwa akionea wivu mafanikio ya mwezie hasa Vidal ambaye amekuwa akilalamika kuwa vyombo vya habari vya Chile vimekuwa vikimpendelea zaidi Alexis Sanchez na kumpuuza yeye hata afanye zuri kiasi gani.

    Siri ya uadui huo imeibuka hivi karibuni baada ya nyota hao kujibizana kupitia mtandao wa twitter baada ya Vidal kuandika 

    "Hahahaha watu wachache sana Chile huongelea soka wakati Mfalme Vidal anapokuwa ameshinda".(Akimaanisha kuwa watu wachache wameongelea ushindi wa goli 5-1 iliyoupata klabu yake ya Bayern Munich dhidi ya Arsenal inayochezewa na Sanchez tofauti na ushindi wa goli 2-0 iliyoupata Arsenal dhidi ya Bayern Munich)

    Sanchez "Katika maisha kuna kushinda,kushindwa nk... .na maisha yanaendelea na unapambana tena.Lakini mtu makini ni yule anayeanguka,akainuka,akajikagua akatabasamu na kisha kusema mapambano yanaendelea"

    La Tercera limeongeza nyota hao wamekuwa na tabia ya kutaka kuwa juu ya wenzao.Wamekuwa wakishindana kununua magari ya kifahari na wakati mwingine wamekuwa wakishindana hata juu ya nani anatoka na mwanamke mzuri.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VIDAL,SANCHEZ URAFIKI KWISHA,WIVU WADAIWA KUWA CHANZO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top