Nairobi,Kenya.
Ubingwa mtamu bwana!!Mashabiki wa Gor Mahia " K'Ogalo" eti wanataka kukipiga na mabingwa wa ligi kuu nchini England Chelsea.Kama si dharau ni nini?
Baada ya kumaliza msimu wa 2014/2015 bila kupoteza mchezo wowote katika ligi kuu ya Kenya sasa mashabiki wa Gor Mahia wanaamini klabu yao ina ubavu wa kuvaana na Chelsea bila tatizo lolote na kuibuka na ushindi kama vifanyavyo vilabu vingine vya nje na ndani ya England kwani wanaamini hivi sasa Chelsea imekuwa kibonde sana.
Mashabiki hao waliokuwa wamejazana katika uwanja wa Nyayo wakiishuhudia klabu yao ikiibamiza Muhoroni Youth mabao 2-0 na kuhitimisha msimu bila kufungwa walionyesha bango lisemalo "sasa tunaitaka Chelsea"
0 comments:
Post a Comment