Munich,Ujerumani.
Unamfahamu yule kiungo wa shoka wa Bayern Munich,Mchile Arturo Vidal "Kiduku"??Basi jamaa ameichimba bonge la mkwara Arsenal akidai kuwa ikitua Allianz Arena jumatano usiku ni kichapo tu hatuna kingine.
Akiongea na gazeti la Bild,Vidal ameionya Arsenal kuwa katika mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa jumatano hii huko Munich,Ujerumani klabu yake ya Bayern Munich haitakuwa na huruma kwa Arsenal zaidi ya kuishushuia kichapo kikali.
Amesema "Tutaionyesha Arsenal kuwa sisi ni nani,tutawaonyesha Bayern Halisi.Kwa sasa morali yetu iko juu.Tutatumia kila nafasi tukayopata na kuhakikisha tunavuna pointi zote tatu"
Kesho kutwa jumatano Bayern Munich itakuwa katika dimba lake la nyumbani kuialika Arsenal katika mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi wa kundi F.Katika mchezo wa kwanza Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment