728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 02, 2015

    HIVI NDIVYO AZAM FC ILIVYOIENGUA YANGA KILELENI MWA VPL



    Azam FC imerejea kileleni baada ya kuitwanga Toto African kwa mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, jana jumapili.

    Azam FC sasa imefikisha pointi 25 na kurejea kileleni juu ya Yanga yenye pointi 23.
    Mabao ya Azam FC ambayo ilitawala mchezo leo yalifungwa na Mrundi Didier Kavumbagu aliyefunga mawili na beki Shomari Kapombe naye akapachika mawili huku moja likifungwa na Kipre Tchetche.
    Wenyeji ndiyo waliotawala mchezo kwa muda wote kuhakikisha mambo yanakwenda safi kwao na wanarejea kileleni baada ya kushushwa na Yanga kwa saa kadhaa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIVI NDIVYO AZAM FC ILIVYOIENGUA YANGA KILELENI MWA VPL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top