Kigali,Rwanda.
MJERUMANI Antoine Hey ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Rwanda maarufu kama 'Amavubi' ama Manyigu.
Taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Rwanda,Ferwafa imesema Hey,46, amepata wadhifa huo baada ya kufanya vyema kwenye usaili uliofanyika Jumatatu ya wiki hii.
Wengine walioshiriki kwenye usaili huo na kutoka mikono mitupu ni Mswisi Raoul Savoy pamoja na Mreno José Rui Lopes Águas.
Kabla ya kupata kibarua hicho,Hey pia aliwahi kufanya kazi katika mataifa ya Lesotho,Gambia, Liberia na Kenya.Jukumu lake kubwa litakuwa ni kuhakikisha Rwanda inarejea kwenye mstali baada ya kupepesuka kwa muda mrefu.
Ikumbukwe Rwanda haijafuzu kwenye michuano mikubwa tangu ilipofanya hivyo mwaka 2004 pale ilipofuzu kwenye michuano ya AFCON na kutolewa kwenye hatua ya makundi.
Rwanda imekuwa haina kocha wa kudumu tangu Agosti mwaka jana baada ya Jonny McKinstry kutoka Wales kufutwa kazi kwa madai ya kushindwa kuipa timu hiyo matokeo mazuri uwanjani.
0 comments:
Post a Comment