728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 05, 2016

    TANZANIA BADO YACHECHEMEA VIWANGO VYA UBORA WA SOKA DUNIANI,ARGENTINA YAONGOZA

    Shirikisho la soka duniani FIFA, limetangaza orodha ya mataifa bora duniani mwezi wa Aprili.

    Kiduniani, Argetina ni ya.kwanza, ikifuatwa na Ubelgiji. Nafasi ya tatu imeiendea Chile,nafasi ya nne Colombia huku Ujerumani ikifunga tano bora.

    Barani Afrika, Algeria ni ya kwanza lakini ya 33 duniani. Cote Dvoire ni ya pili huku ikiwa ya 34 duniani, huku Ghana ikishika nafasi ya tatu barani Afrika lakini ni ya 38 duniani.

    Senegal ni ya nne, Misri ya tano, Cape Verde ya sita barani Afrika na ya 47 duniani huku Tunisia ikiwa ya saba wakati DRC ikifunga nane bora barani Afrika lakini inashikilia nafasi ya 51 duniani.

    Uganda inaendelea kuongoza katikaukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, na ni ya 16 barani Afrika na ya 72 duniani.

    Rwanda ni ya pili, 21 barani Afrika na 87 duniani. Kenya ni ya tatu, inashikilia nafasi 33 barani Afrika na ya 116 duniani. Burundi ni ya 37 barani Afrika na ya 123 duniani. Tanzania nayo ni ya 41 barani Afrika huku ikiwa ya 129 duniani.Djibouti, Eritrea na Somalia zinashikilia nafasi ya mwisho katika orodha ya mwezi huu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TANZANIA BADO YACHECHEMEA VIWANGO VYA UBORA WA SOKA DUNIANI,ARGENTINA YAONGOZA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top