728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 05, 2016

    UZEMBE WAIPONZA AZAM FC YAPOKONYWA POINTI TATU LIGI KUU

    Dar es salaam,Tanzania.

    TIMU ya Azam FC, imepokonywa pointi tatu na mabao matatu kutokana na kumtumia beki wao, Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.

    Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sokoine,Mbeya, Azam ilimchezesha Nyoni kinyume na sheria huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

    “Azam wamepoteza mchezo ule na sasa Mbeya City imepewa pointi tatu na mabao matatu pia tumelipa onyo benchi la ufundi la Azam kuwa makini ili jambo hili lisiwatokee tena,” alisema Lucas.

    Baada ya kukatwa pointi tatu sasa Azam wameshushwa nafasi moja kutoka nafasi ya pili hadi ya tatu huku wakiwa na alama 57 na nafasi ya pili ikipanda Simba ambayo ina alama 58.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UZEMBE WAIPONZA AZAM FC YAPOKONYWA POINTI TATU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top