728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    JOGOO LIVERPOOL LATINGA FAINALI EUROPA LIGI SASA KUVAANA NA MABINGWA WATETEZI SEVILLA,MSHINDI KUCHEZA LIGI YA MABINGWA

    Liverpool ,England.

    Liverpool imetinga fainali ya michuano ya Europa Ligi baada ya Alhamis usiku kuichapa Villarreal kwa mabao 3-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali ya pili uliopigwa katika uwanja wa Anfield,Liverpool.

    Mabao yaliyoipeleka Liverpool fainali yamefungwa na Bruno Soriano aliyejifunga,Daniel Sturridge na Adam
    Lallana.Kwa matokeo hayo Liverpool imefuzu kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya mchezo wa kwanza kuchapwa bao 1-0 huko El Madriga,Hispania.

    Liverpool imetinga fainali baada ya kuving'oa vigogo vya soka Ulaya kama Augsburg, Manchester
    United, Borussia Dortmund na Villarreal.Fainali ijayo itakuwa ni ya kwanza kwa kwa miamba hiyo ya Anfield tangu mwaka 2007.

    Katika mchezo mwingine wa nusu fainali uliopigwa huko Ramon Sanchez Pizjuan mabingwa watetezi Sevilla wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuichapa Shakhtar Donetsk kwa mabao 3-1.Shukrani kwa mabao ya Mfaransa Kevin Gameiro aliyefunga mara mbili na Mariano.Kwa matokeo hayo Sevilla imefuzu kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya mchezo wa kwanza kuisha kwa sare ya mabao 2-2.

    Mchezo wa fainali utachezwa Mei 18 huko Basel,Uswisi na mshindi wa mchezo licha ya kupata kikombe pia atakuwa amefuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JOGOO LIVERPOOL LATINGA FAINALI EUROPA LIGI SASA KUVAANA NA MABINGWA WATETEZI SEVILLA,MSHINDI KUCHEZA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top