728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    OSCAR,NEYMAR JR WATEMWA KIKOSI CHA BRAZIL

    Rio de Janeiro,Brazil.

    Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Carlos Dunga ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya kombe la Copa America
    Centenario itakayoanza kutimua vumbi lake mwezi Juni mwaka huu huko Marekani.

    Katika kikosi hicho Dunga amewatema jumla ya wachezaji 17 kutoka kikosi cha awali cha wachezaji 40.Wachezaji waliotemwa ni pamoja na Ricardo Kaka, Roberto Firmino, Lucas Moura na Oscar Dos Santos.

    Wengine ni Marcelo Grohe, Fagner,Alex Sandro, Jemerson, Gabriel Paulista,Wallace, Fernandinho, Ganso, FelipeAnderson, Luan, Jonas, Alex Teixeira,Gabriel Jesus pamoja na nahodha Neymar Jr ambaye kutemwa kwake kumetoka na maombi ya klabu yake ya FC Barcelona
    kutaka nyota huyo apumzishwe.

    Brazil imepangwa kundi B pamoja na mataifa ya Ecuador Haiti na Peru.Michuano ya Copa America Centenario imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 100 ya uhai wa chama cha soka cha Amerika ya Kusini na itashirikisha jumla ya 16 badala ya 12 kama ilivyozoeleka.Mataifa sita ya Amerika ya Kaskazini (CONCACAF) na kumi ya Amerika Kusini (CONMEBOL)

    Kwa mara ya kwanza michuano hiyo itafanyika nje ya bara la Amerika ya Kusini kuanzia Juni 3-26,2016.

    KIKOSI KAMILI CHA BRAZIL

    Makipa : Alisson (Internacional), Diego Alves (Valencia), Ederson (Benfica)

    Walinzi : Miranda (Inter), Gil (Shandong Luneng), Marquinhos (Paris Saint-
    Germain), Rodrigo Caio (Sao Paulo), Dani Alves (Barcelona), Filipe Luis (Atletico Madrid), Fabinho (Monaco), Douglas Santos (Atletico Mineiro)

    Viungo: Luiz Gustavo (Wolfsburg), Elias (Corinthians), Renato Augusto (Beijing
    Guoan), Coutinho (Liverpool), Lucas Lima (Santos), Willian (Chelsea), Casemiro (Real
    Madrid), Rafinha (Barcelona)

    Washambuliaji : Douglas Costa (Bayern Munich),Hulk (Zenit), Gabigol (Santos), Ricardo Oliveira (Santos)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OSCAR,NEYMAR JR WATEMWA KIKOSI CHA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top