728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    BOSI WA TP MAZEMBE AUTAKA URAIS CONGO

    Lubumbashi,Congo.

    Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe bilionea Moise Katumbi Chapwe ametangaza kuwa atagombea kiti cha Urais wa Congo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

    Katumbi,51 ambaye ni gavana wa zamani wa jimbo la Katanga ametoa taarifa hiyo kupitia ukurusa wake rasmi wa twitter na kuweka wazi kuwa atagombea kiti hicho kwa tiketi ya upinzani kufuatia kuombwa kufanya hivyo.

    Katumbi alijiunga na upinzani Septemba 2015 muda mfupi baada ya kujiuluzu ugavana wa jimbo la Katanga.

    Katumbi anatarajiwa kupata upinzani kidogo katika uchaguzi huo hasa baada ya kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo Joseph Kabila hatagombea kwa kuwa muda wake wa kukaa madarakani umeshakwisha.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BOSI WA TP MAZEMBE AUTAKA URAIS CONGO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top