728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    DANNY LYANGA ATIBUA HESABU ZA SIMBA

    Dar es salaam,Tanzania.

    SIMBA imepata pigo baada ya mshambuliaji wake, Danny Lyanga, kutakiwa kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kufuatia kupata maumivu ya goti la kulia.

    Lyanga alipata jeraha hilo la goti katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa kutoka suluhu ya 0-0.

    Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, amesema Lyanga alipelekwa katika Hospitali ya Agakhan kwa
    ajili ya uchunguzi na kugundulika kuwa ni majeruhi.

    Gembe amesema Simba inaweza kumkosa mshambuliaji mwingine Hijja Ugando, katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa.Alisema mshambuliaji huyo alichanika sehemu ya kichwa na kushonwa nyuzi tatu wakati akicheza dhidi ya Azam.

    Kwa maana hiyo Simba itakazimika kuwategemea washamnuliaji Hamisi Kiiza Ibrahim Ajib na mkongwe Mussa Mgosi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DANNY LYANGA ATIBUA HESABU ZA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top