728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    HIVI HAPA HABARI 11ZA USAJILI BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO APRILI 6,2016

    Vincent Janssen

    Na sokaextra.blogspot.com

    Janssen:Arsenal imeripotiwa kuwa katika mawindo ya kukiimarisha kikosi chake baada ya kudaiwa kuanza kumfuatilia kwa ukaribu zaidi mshambuliaji wa AZ Alkmaar ya Uholanzi Vincent Janssen.Janssen,21 ameifungia AZ Alkmaar mabao 26 katika michezo 33 ya ligi ya Eredivisie tangu ajiunge nayo msimu huu akitokea Almere City.(Daily Telegraph)

    Mahrez:Wakala wa winga Riyad Mahrez anayeitwa Kamel Bengougam amesema kuna nafasi finyu sana kwa mteja wake kubaki Leceister City kutokana na kuwindwa na na vilabu vingi vikubwa.(The Guardian)

    Mourinho:Jose Mourinho amekataa kusubiri mpaka mwaka 2017 ndipo apate nafasi ya kujiunga na Manchester United hii ni baada ya klabu hiyo ya Old Trafford kuweka wazi kuwa kwa sasa haina mpango wa kuachana na kocha wake wa sasa Mholanzi Louis van Gaal.(Daily Mail)

    Lapadula:Rais wa Pescara Daniele Sebastiani amedai kufanya mazungumzo na kocha wa Leicester City Claudio Ranieri kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake Mperu Gianluca Lapadula.Lapadula ameifungia Pescara mabao 20 katika ligi ya Seria B.(Tutto Mercato)

    Stegen:Mlinda mlango wa Barcelona Mjerumani Marc-Andre ter
    Stegen amesema hana mpango wa kuhama klabu huyo licha ya kutakiwa na klabu ya Liverpool.(Liverpool Echo)

    Ben Arfa:Hatem Ben Arfa anatarajiwa kujiunga na Barcelona msimu ujao akiwa kama mchezaji baada ya kufanya vizuri katika klabu yake ya sasa ya Nice.Ben Arfa amepewa nafasi kubwa kuwapiku Kevin Gameiro na Alexandre Lacazette ambao nao wamekuwa wakiwindwa na miamba hiyo ya Hispania.(L'Equipe)

    Kane:Harry Kane anakaribia kusaini mkataba mpya katika klabu yake ya Tottenham.Mkataba huo mpya utamuwezesha Kane kupokea mshahara wa £100,000 kwa wiki na kuwa mchezaji anayelipwa vizuri katika historia ya klabu hiyo.(Daily Mirror)

    Lookman:Liverpool imeungana na vilabu vya Chelsea, Tottenham,
    Arsenal na Everton katika mbio za kumuwania mshambulia kinda wa Charlton Athletics Ademola Lookman,18 mwenye thamani ya £6m.(Daily Mirror)

    Courtois:Mlinda mlango Thibaut Courtois huenda akaihama Chelsea baada ya kudaiwa kugombana na kocha wa makipa wa klabu hiyo Mfaransa Christophe Lollichon.Habari zaidi zinasema Courtois amesema atabaki Chelsea ikiwa kocha huyo atatimuliwa.(The Sun)

    Van Gaal:Manchester United italazimika kumlipa kitita cha £5m kocha wake mkuu Mholanzi Louis Van Gaal ikiwa itataka kuvunja mkataba nae ili imtwae Mreno Jose Mourinho.(The Sun)

    Batshuayi: West Ham huenda ikavunja rekodi ya usajili baada ya kuripotiwa kutenga kitita cha £31.5m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Marseille Michy Batshuayi.Batshuayi pia inawindwa na vilabu vya Juventus, Roma na Tottenham.(The Guardian)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIVI HAPA HABARI 11ZA USAJILI BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO APRILI 6,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top