London,England.
SIRI IMEFICHUKA.Mshambuliaji Diego Costa amesema sababu ya yeye kushindwa kuwika msimu huu kumesababishwa na kuongezeka uzito kulitokana na kunenepa kupita kiasi.
Akifanya mazungumzo na mtandao wa Chelsea,Costa amekiri kula hovyo wakati wa likizo kitendo ambacho kimemfanya awe mzito uwanjani.Amesema
"Nilipata jeraha mwishoni mwa msimu uliopita,nikaenda likizo.Nadhani niliteleza katika ulaji.Niliporudi klabuni sikuwa Costa yule wa siku zote,nilikuwa mzito hali ambayo imenifanya nishindwe kufanya vizuri uwanjani"
Akijibu swali aliloulizwa juu ya mwenendo mbaya wa Chelsea ,Costa amesema "Lawana na shutuma zote zinapaswa ziende kwa sisi wachezaji na siyo kocha.Kocha anafanya kazi yake vizuri,anajitahidi lakini wachezaji ndiyo tunaomwangusha.Tulipotoka likizo tulijiamini kupita kiasi,tulidhani mambo yangekuwa kama ya msimu uliopita lakini hali imekuwa ni tofauti kabisa.Tunajipanga,tunafanya mazoezi kwa bidii ili turudi katika makali yetu yaliyozoeleka"
Mpaka sasa Costa amefunga bao moja pekee katika michezo tisa hali iliyopelekea kutemwa katika kikosi cha Hispania.
0 comments:
Post a Comment