MAWAKALA wa kimataifa wanaotambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), wametua nchini kwaajili ya kuwafuatilia wachezaji chipukizi walio kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars, wakiwamo Said Ndemla, Farid Mussa na kipa mahiri,Ally Mustapha ‘Barthez’.
Mawakala hao walikuwapo kwenye mechi kati ya Taifa Stars na Malawi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi ya kuwania kupangwa katika makundi ya kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia zilizopangwa kufanyika 2018 nchini Urusi.
Katika mechi hiyo, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0,
wafungaji wakiwa ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wanacheza
soka ya kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).
Baadhi ya mawakala hao, wapowanaotoka Afrika Kusini, Zambia, Malawi ambao hata hivyo, hawakuwa tayari kutaja majina yao, lakini wakiweka wazi kuvutiwa na Ndemla ambaye ni kiungo wa Simba, Farid wa Azam FC, Barthez wa Yanga, Himid Mao na Shomari Kapombe wa Azam.
Walisema walivutiwa na uchezaji wa wachezaji hao ikizingatiwa bado wanaumri mdogo, huku Barthez pamoja na kuwa na umri mkubwa akionekana kuwa ni kipa mzoefu katika mechi za kimataifa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, alisema zaidi ya mawakala saba walikuwepo kwenye mechi hiyo kwa ajili ya kufuatilia vipaji vya soka kwa wachezaji wa Taifa Stars.
Malinzi alisema baadhi ya mawakala walipitia TFF na kujitambulisha juu ya ujio wao nchini kwa ajili ya kuwafuatilia wachezaji wenye vipaji vya kucheza soka.
“Kulikuwa na mawakala wengi kama alivyosema rais, lakini kuna baadhi walipitia kwetu kujitambulisha, sheria ya Fifa inakataza kutaja majina yao,” alisema Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.
(CHANZO:BINGWA)

0 comments:
Post a Comment