Lagos,Nigeria.
Mlinda mlango Vicent Enyeama ameachana na timu ya taifa ya Nigeria baada ya kuitumikia kwa miaka 13 kufuatia kutokea msuguano kati yake na kocha Sunday Oliseh.
Enyeama,33 amefikia uamuzi huo jana alhamisi baada ya kuvuliwa unahodha kufuatia kuchelewa kuripoti kambini huko Ubelgiji.Enyeama alichelewa kufika kambini kufuatia kuhudhuria mazishi ya mama yake mzazi aliyefariki dunia hivi karibuni.
Enyeama akiwajibika langoni mwa Super Eagles
Taarifa zinasema kuchelewa huko kwa Enyeama kulimkasirisha kocha Sunday Oliseh ambaye aliamua kumkabidi kitambaa cha unahodha kiungo Mustafa Musa na hata Enyeama alipowasili kambini hakuruhusiwa kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzie kitendo kilichomkera na kuamua kuachana na timu hiyo baada ya kuichezea michezo 101.
0 comments:
Post a Comment