London,England.
Wayne Rooney atakuwa jukwaani akiitazama England ikivaana na Estonia leo usiku katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) baada ya kuwa na tatizo la kifundo cha mguu (enka).
Kufuatia kuuumia kwa Rooney,Kocha Roy Hodgson amepanga kumtumia Harry Kane kama mshambuliaji huku Theo Walcot na Raheem Sterling wakicheza pembeni yake.Wakati Rooney akiwa nje,kiungo Michael Carrick yeye anasubiri taarifa za madaktari ili kujua kama atacheza ama la.
Kikosi cha England kitakachoshuka dimbani Wembley leo ni hiki hapa
Hart; Clyne, Cahill, Smalling, Bertrand; Carrick/Barkley, Milner, Lallana; Walcott, Sterling, Kane.
Timu ambazo zimefuzu tayari katika michuano hiyo ni Czech Republic, England, Austria, Northern Ireland, Portugal and - unexpectedly - Iceland.
0 comments:
Post a Comment