728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 09, 2015

    RASMI:KLOPP ASAINI MIAKA MITATU LIVERPOOL,APANGUA BENCHI LA UFUNDI KAMA CHIZI VILE

    Liverpool,England.

    Jurgen Klopp sasa ndiye kocha mpya wa Liverpool baada ya kumwaga wino wa kuifundisha miamba hiyo ya Anfield kwa misimu mitatu.Klopp amejiunga na Liverpool akichukua nafasi ya kocha aliyetimuliwa klabuni hapo Brendan Rodgers kufuatia kuonyesaha mwenendo mbaya katika ligi kuu.
    Confirmed: Liverpool appoint Jurgen Klopp's assistants Zeljko Buvac and Peter Krawietz
    Zeljko Buvac
    Kufuatia mkataba huo Klopp atakuwa akilipwa kitita cha paundi milioni 7.37 kwa mwaka.Taarifa kutoka ndani ya Liverpool zinasema Klopp ameanza kukiksuka kikosi chake baada ya kulipangua benchi lote la ufundi lililokuwa chini ya Rodgers.Kocha msaidizi O'Driscoll ameondolewa, huku McAllister akibadilishiwa majukumu,Pepijn Lijnders ataendelea kubaki.Pia Klopp anatarajia kuwaongeza Zeljko Buvac na Peter Krawietz kutoka Borussia Dortmund kama wasaidizi wake.
    Confirmed: Liverpool appoint Jurgen Klopp's assistants Zeljko Buvac and Peter Krawietz
    Peter Krawietz
    Mtihani wa kwanza kwa Klopp akiwa na Liverpool itakuwa ni kupata ushindi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa ligi kuu jumamosi October 17.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RASMI:KLOPP ASAINI MIAKA MITATU LIVERPOOL,APANGUA BENCHI LA UFUNDI KAMA CHIZI VILE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top