728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 10, 2015

    TP MAZEMBE YAJA NCHINI KUZIBOMOA YANGA,AZAM

                         
    MABINGWA wa zamani wa Afrika, TP Mazembe, wanatarajiwa kutua nchini kesho ambapo pamoja na mambo mengine, watawachunguza kwa karibu zaidi nyota kadhaa waliotamba kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, wakiwamo Geoffrey Mwashiuya na Malimi Busungu wa Yanga.

    Kwa mujibu wa habari zilizotufikia juzi, miamba hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imeonekana kuvutiwa na wachezaji hao kutokana na viwango vyao, wakiwamo Pascal Wawa, Mussa Farid na wengineo wa Azam.

    Mtu wa karibu na timu hiyo wanayochezea Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, alisema kuwa mabosi wa TP Mazembe wamevutiwa na baadhi ya wachezaji wa Yanga na Azam waliocheza Kagame wakipata picha kuwa Tanzania imesheheni vipaji vya soka hivyo ni vema wakaelekeza nguvu zao ili kuviendeleza.


    “Kombe la Kagame ni neema kwa wachezaji wa Tanzania, (mabosi wa TP Mazembe) walikuwa wakifuatilia sana mashindano hayo na kugundua vipaji vingi tu, wakiwamo Busungu, Geoffrey, Deus Kaseke pamoja na wengine kutoka Azam, wakimtaja pia Wawa raia wa Ivory Coast,” alisema mtoa habari wetu huyo ambaye hakutaka jina lake kuwekwa hadharani.


    Alisema TP Mazembe wamebaini kuwa wanaweza kupata wachezaji wenye umri mdogo kutoka Tanzania na kuwaendeleza kwa maslahi ya klabu yao kama wanavyonufaika na akina Samatta na baadaye kuwauza Ulaya.


    (BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TP MAZEMBE YAJA NCHINI KUZIBOMOA YANGA,AZAM Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top