
WACHEZAJI wapya wa Simba akiwamo Mganda, Hamis Kiiza, wamejikuta mikononi mwa URA ya Uganda watakayocheza nayo Jumamosi hii ili kuwapima zaidi, ukiwa ni mchezo wa kirafiki kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu, ikiwa ni baada ya mechi ya Ngao ya Jamii kati ya mabingwa Yanga na washindi wa pili, Azam FC.
Akizungumza mara baada ya kikosi chao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya SC Villa ya Uganda, Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema mchezo huo wa Jumamosi ni nafasi nyingine kwa nyota wao wapya kudhihirisha ubora wao mbele ya benchi la ufundi na mashabiki.
Alisema lengo la michezo hiyo ni kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa fiti kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
0 comments:
Post a Comment