Rio de Janeiro,Brazil.
MWANARIADHA wa Jamaica,Usain Bolt, ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mwamba katika mchezo huo baada ya leo alfajiri kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 200 kwa upande wa wanaume akitumia sekunde 19.78.
Nafasi ya pili imeenda kwa Andre de Grasse wa Canada aliyekimbia kwa sekunde 20.02.Nafasi ya tatu imeenda kwa Christophe Lemaitre wa Ufaransa aliyekimbia kwa kasi ya sekunde 20.12.
Kabla ya kutwaa medali ya mita 200 tayari Bolt alikuwa ameshatwaa medali ya dhabu ya mita 100.Medali hizo mbili zinamfanya Bolt awe mwanariadha wa kwanza kuwahi kushinda medali mbili za dhahabu katika michuano mitatu mfululizo ya Olimpiki sawa na medali sita,mita 100 medali tatu, mita 200 medali tatu.
Rekodi
2008 Beijing – 100m dhahabu, 200m dhahabu.
2012 London – 100m dhahabu, 200m dhahabu.
2016 Rio – 100m dhahabu, 200m dhahabu.
Bolt atarejea tena dimbani Ijumaa katika mbio za mita 4×100 kupokezana vijiti.Mbio ambazo kushinda kwake kutategemea kasi ya wenzie.
0 comments:
Post a Comment