728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 21, 2016

    UEFA YATAJA 18 WALIOFANYA VIZURI  EUROPA LIGI,ENGLAND YATOA WANNE TU

    Basel, Uswisi. 

    SHIRIKISHO la vyama vya Soka Barani Ulaya (UEFA) limetangaza kikosi cha wachezaji 18 waliofanya vizuri zaidi katika michuano yake ya Europa Ligi iliyoisha hivi karibuni kwa Sevilla kutwaa ubingwa baada ya kuifunga Liverpool kwa mabao 3-1 huko St Jakob Park,Basel-Uswisi. 

    Katika kikosi hicho Mabingwa Sevilla wametoa wachezaji saba huku Ligi Kuu ya England ikifanikiwa kutoa wachezaji wanne pekee.Wachezaji hao ni David De Gea,Philippe Coutinho,Toby Alderweireld na Emre Can  

    Ujerumani imetoa wachezaji watatu,Hispania tisa na Ukraine wawili . 

    KIKOSI KAMILI 

    Makipa:David Soria (Sevilla)
    David De Gea (Manchester United)

    Mabeki:Toby Alderweireld (Tottenham Hotspur),Mats Hummels (Borussia Dortmund),Adil Rami (Sevilla),Mariano (Sevilla),Darijo Srna (Shakhtar Dontesk)

    Viungo:Emre Can (Liverpool),Gonzalo Castro (Borussia Dortmund),Philippe Coutinho (Liverpool),Ever Banega (Sevilla),Grezegorz Krychowiak (Sevilla),Steven N’Zonzi (Sevilla),Marlos (Shakhtar Donetsk)

    Washambuliaji:Aritz Aduriz (Athletic Bilbao),Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund),Cedric Bakambu (Villarreal) na Kevin Gameiro (Sevilla)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UEFA YATAJA 18 WALIOFANYA VIZURI  EUROPA LIGI,ENGLAND YATOA WANNE TU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top