Paris,Ufaransa.
STAA wa Manchester United,Paul Pogba amepata pigo baya maishani baada ya kufiwa na baba yake mzazi Mzee Fassou Antoine Pogba huko Paris,Ufaransa.
Fassou amefariki jana Ijumaa akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Fassou aliondoka nyumbani kwao Guinea na kuhamia Ufaransa akiwa na umri wa miaka 30.
Kabla ya kifo chake Fassou alikuwa mcheza soka kama ilivyo kwa wanawe Paul,Florentin na Mathias.Safari yake ya kisoka ilianzia nchini kwake Guinea kabla ya kutimkia nchini Ufaransa ambako alibahatika kupata kazi kwenye shirika moja la mawasiliano ya simu huku akicheza soka.
Baada ya kustaafu soka Fassou alianza kujihusisha na kufundisha soka watoto wake na wa maeneo ya jirani na nyumbani kwake.
"Nilicheza soka katika levo iliyokuwa ndogo kuliko levo niliyotamani kucheza.Fassou aliwahi kuliambia Telegraph mwaka 2016.
Nilitaka watoto wangu wacheze soka kwenye levo ya juu zaidi kuliko ile niliyocheza mimi.Nilikuwa mkali sana kwao wakati wakiwa wadogo hali hiyo iliwafanya wajue mambo haraka.
0 comments:
Post a Comment