Dortmund,Ujerumani.
AS MONACO imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya usiku wa leo ikiwa ugenini kuifunga Borussia Dortmund kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park huko Dortmund.
Kinda Mfaransa Kylain Mbappe Lottin (18) ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo wa leo baada ya kuifungia AS Monaco mabao mawili katika dakika za 19 na 79.Bao la tatu la AS Monaco limefungwa na Sven Bender aliyejifunga katika dakika ya 35 ya mchezo.
Mabao ya wenyeji Borussia Dortmund yamefungwa na Oussame Dembele katika dakika ya 57.Bao la pili limefungwa na Mjapan,Shinji Kagawa katika dakika ya 84.
Aidha katika mchezo huo uliokuwa uchezwe jana na badala yake ukaahirishwa baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu, ilishuhudiwa Fabinho wa AS Monaco akishindwa kuiandika bao klabu hiyo baada ya kukosa mkwaju wa penati katika dakika za mwanzoni.
0 comments:
Post a Comment