Faridi Miraji, Dar es salaam.
Golikipa Msomi wa Mbao FC, Erick Ngwengwe amesimamishwa kuichezea timu hiyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za kuihujumu timu yake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba. Katika mchezo huo uliochezwa Jumatatu Mbao walikuwa mbele kwa mabao mawili Kwa bila (2-0) mpaka Dakika ya 81 baadae Simba waliweza kurudisha mabao yote mawili na kuongeza la Ushindi mpaka mwisho wa mchezo simba walishida Kwa mabao matatu Kwa mbili (3-2)
Baada ya Mchezo huo mashabiki wa Mbao FC waliibua taarifa ya kipa Wao amehujumu timu Kwa Madai ya kupokea rushwa kutoka Simba . Mashabiki wa Mbao hawakuishia hapo kesho yake baada ya mechi yaani Jumanne Walienda kuushinikiza uongozi kumfukuza Erick Ngwengwe Kwa kufungisha.
Baada ya sekeseke hilo mwenyekiti wa Mbao FC,Solly Njachi amedhibitisha kumsimamisha kipa wao Erick Ngwengwe '' Ni kweli Uongozi umemsimaisha mchezaji Erick Ngwengwe kupisha uchunguzi wa tuhuma za kupokea rushwa na akibainika kweli basi ataodolewa kwenye timu "
Alisema Solly
0 comments:
Post a Comment