Dar es salaam,Tanzania.
Mlinzi na nahodha wa zamani wa Taifa Stars Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesisitiza kamwe hawezi kula matapishi yake na kurejea kuichezea tena timu hiyo licha ya kujumuishwa na Kocha Boniface Mkwasa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoingia kambini Mei 23 kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri Juni 4.
Cannavaro amesema uamuzi wake wa kujiengua kuichezea Taifa Stars hautabadilika na wala hatarajii tena kujiunga na kikosi hicho.
Mapema mwaka huu Cannavaro alitangaza kustaafu kuichezea Taifa Stars baada ya Kocha Boniface Mkwasa kumvua kitambaa cha unahodha na kumpa Mbwana Samatta
kama zawadi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika.
0 comments:
Post a Comment