Dar es salaam,Tanzania.
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Wawakilishi pekee wa Michuano ya Kimataifa kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki,Yanga SC imefungua rasmi mazungumzo na Kocha wake Mkuu Mholanzi Hans Van Pluijm kuhusu Mkataba
mpya baada ya ule wa sasa kubakisha takribani siku chache tu ufikie mwisho.
Habari zilizoifikia SOKA EXTRA zinasema kwamba Yanga SC inataka kumpa Pluijm mkataba mnono zaidi ya ule wa sasa na utakaokuwa mrefu mpaka achoke mwenyewe kama ilivyo kwa kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger Wenger ambaye ana miaka ishirini klabuni hapo.Kilisema chanzo hicho.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Pluijm kuipa Yanga SC ubingwa wa pili mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na kuipeleka hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kufuatia kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1.Yanga SC inataka kulipa fadhira kwa kumpa mkataba mrefu zaidi.
0 comments:
Post a Comment