Dar es salaam,Tanzania.
KLABU ya Azam FC imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji hatari wa timu ya Zesco ya Zambia raia wa Kenya,
Jesse Were, kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake msimu ujao.
Were ameonyesha kuwavutia mabosi wa Azam ambapo hivi sasa mabosi hao wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu
mshambuliaji huyo kwa ajili ya kumshawishi kumsajili.
Itakumbukwa Were ndiye aliyefunga bao la pili na kuiwezesha timu yake ya Zesco United kupata ushindi wa kwanza ilipoichapa Nchanga Rangers mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zambia mapema wiki hii.
Were ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Tusker FC ya Kenya,amefikisha jumla ya mabao 10 msimu huu katika Ligi Kuu nchini Zambia na kumfanya kuwa mmoja wa washambuliaji hatari katika kikosi cha Zesco.
Zesco ilipata ushindi huo baada ya kupoteza michezo minne mfululizo ikiwa ni rekodi mbovu tangu mwaka 2011, ilicheza kwa kujiamini na kuichapa Rangers ambayo haijawahi kuibuka na ushindi dhidi ya Zesco katika dimba la Nchanga tangu mwaka 2004.
Wakala wa mchezaji huyu aliyepo Nairobi,George Bwana, amekiri kupigiwa simu na viongozi wa klabu ya Azam wakimtaka kijana huyo.
“Nathibitisha kupigiwa simu kadhaa kutoka Tanzania kuhusu dili la Were wakitaka kumchukua kwa shilingi milioni 10 (zaidi ya milioni 100 za Tanzania),” alisema Bwana.
0 comments:
Post a Comment