728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 22, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAPILI YA LEO MEI 22,2016.


    Na sokaextra.blogspot.com

    Sissoko:Arsenal inataka kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kumsajili kiungo wa Newcastle United Mfaransa Mousa Sissoko.Imedaiwa kutenga dau la £10m ili kukamilisha dili hilo.(The Sun)

    Drinkwater:Kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp amedaiwa kuvutiwa na kiungo mkabaji wa Leceister City Danny Drinkwater na yuko tayari kutoa kitita cha £14m ili kumleta Anfield.(Daily Mirror)

    Krychowiak:Manchester United imeripotiwa kuipiku Arsenal katika mbio za kumsajili kiungo wa Sevilla Grzegorz Krychowiak,26 mwenye thamani ya £30m.(The Sun)

    Gotze:Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ana matumaini ya kukamilisha mapema wiki ijayo usajili wa kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze mwenye thamani ya £20m.(The Sun)

    Koulibaly:Chelsea inaandaa ofa inayodhaniwa kukaribia €25m ili kumsajili mlinzi wa kati wa Napoli Msenegal Kalidou Koulibaly.(Gazzetta dello Sport)

    Rulli:Manchester City inakaribia kumsajili mlinda mlango wa Real Sociedad Geronimo Rulli ili kuziba nafasi ya mlinda mlango wake Willy Caballero anayetaka kuondoka Etihad Stadium.(Daily Mail)

    Mane:Arsenal itajaribu kumsajili winga wa Southampton Sadio Mane,23 kwa ada ya £17m ($24m) ikiwa winga wake Alex Oxlade-Chamberlain,22 atajiunga na Leceister City inayodaiwa kumtaka.(The Mirror) 

    Oxford:Manchester United iko tayari kutoa kitita cha £10m ili kumnasa mlinzi kinda wa West Ham Reece Oxford,17.(The Mirror)

    Mason:Tottenham Hotspurs imeripotiwa kuwa tayari kumuuza kiungo wake asiye na furaha klabuni hapo Ryan Mason,25 kwenda Bournemouth kwa kitita cha £2m.(The Daily Star)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMAPILI YA LEO MEI 22,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top