728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 09, 2016

    SAKHO RUKSA LIVERPOOL,UEFA YAMFUTIA KESI YA MADAWA

    Paris,Ufaransa.

    MLINZI wa Liverpool na Ufaransa,Mamadou Sakho,sasa ruksa kuendelea kucheza soka hii ni baada ya Ijumaa Usiku Shirikisho la soka Barani Ulaya (Uefa) kupitia kamati yake huru ya ya Udhibiti, Maadili na Nidhamu,kifupi CEDB kumfutia mashitaka yaliyokuwa yakimkabiri ya kutumia madawa ya kusisimua misuli.

    Machi 17,2016 katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa michuano ya Europa Ligi katika ya Manchester United na Liverpool ulioisha kwa sare ya bao 1-1,Sakho,26,alipimwa na kugundulika kuwa alitumia madawa ya kuyeyusha mafuta mwilini hali iliyopelekea afungiwe kucheza soka kwa kipindi cha awali cha siku 30 kupisha uchunguzi zaidi.

    Baada ya kujiridhisha na uchunguzi wake katika shauli lililofanyika Paris- Ufaransa,huku Sakho akiwakilishwa na Wakili wake,UEFA kupitia CEDB imemfutia makosa yote yaliyokuwa yakitishia soka la staa huyo wa zamani wa Paris Saint Germain na sasa yuko huru kuitumikia Liverpool na Ufaransa.

    Sakho alijiunga na Liverpool mwaka 2013 kwa kitita cha £18m ($25 million) kutoka Paris Saint Germain.Ameichezea Ufaransa jumla ya michezo 28 na kama siyo kuwa na kesi hiyo huenda kesho Jumapili angekuwa sehemu ya kikosi cha kocha Didier Deschamps kitakachoshuka dimbani huko Saint Denis kuvaana na Ureno katika mchezo wa fainali ya Euro 2016.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAKHO RUKSA LIVERPOOL,UEFA YAMFUTIA KESI YA MADAWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top