Turiani,Morogoro.
KLABU ya Mtibwa Sugar
imethibitisha kukamilisha dili la kumuuza mchezaji wao Shiza Kichuya kwa klabu ya Simba.
Kichuya alitajwa kumezewa mate na Simba kwa muda mrefu ambapo Msemaji wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema kuwa
tayari wamemalizana na klabu na mchezaji ameshajiunga na wekundu
hao wa Msimbazi.
Alisema mchezaji huyo sasa ni mali ya Simba na kwamba wanaangalia namna ya kuziba pengo lake kwa kufanya usajili mwingine kuanzia wiki ijayo.
“Tayari tumekamilisha dili la kumuuza Kichuya, kwa hiyo ameshajiunga na wenzake wa Simba, ni mchezaji mzuri
tunasikitika lakini hatuna jinsi,tutaangalia wengine wa kuziba pengo lake,” alisema.
Kusajiliwa kwa Kichuya kutakamilisha jumla ya wachezaji watatu wakitokea Mtibwa Sugar na kuuzwa katika timu hiyo ya Simba.Wengine ni Mohamed Ibrahim na Muzamil Yasin.
0 comments:
Post a Comment