Santiago,Chile.
PEDRO VAZQUEZ huyu ni shabiki wa soka wa Chile na ndiye anayeumiliki ule mpira uliopigwa na Lionel Messi na kukosa penati katika mchezo wa Fainali ya Kombe la Copa America Centenario mwezi uliopita na Chile kuibuka Mabingwa kwa kuichapa Argentina kwa penati 4-2 huko MetLife Stadium,New Jersey-Marekani.
Mpira huo umeanza kumtia hofu,Vazquez na anafikiria kuupiga mnada kwa kiasi cha Euro 27,000 (Milioni 48 za Tanzania) kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kwa sababu za kiusalama.
Vazquez amekiri kuwa anataka kuupiga mnada mpira huo kabla haujaanza kuwindwa na wezi ama watu wengine wabaya.
Amesema “Ukweli ni kwamba kama mpira utapanda thamani zaidi,basi itakuwa hatari sana kuwa nao nyumbani.Ninaweza kuuza lakini hiyo itategemea na hali itakavyokuwa.
“Ni jambo jema kuendelea kuwa na mpira huu lakini kama utaendelea kupanda thamani,nitaupiga mnada".
Wataalamu wa masuala ya biashara wamesema kuwa ikiwa Vazques ataupiga mnada mpira huo katika miezi inayokuja basi atakuwa na uhakika wa kuvuna kiasi kikubwa zaidi cha pesa bila kuvuja jasho.
0 comments:
Post a Comment