Shanghai, China.
MSHAMBULIAJI Mkongwe wa Senegal,Papiss Demba
Cisse ameihama Newcastle United na kujiunga na Shandong Luneng inayoshiriki ligi kuu ya China kwa ada ya Paundi Milioni 5.
Cisse,31,alijiunga na Newcastle United mwaka 2012 akitokea Freiburg ya Ujerumani kwa ada ya Paundi Milioni 10 amejiunga na Shandong Luneng mchana huu baada ya kufaulu zoezi la upimaji wa afya.
Cisse ameiacha Newcstle United akiwa ameifungia mabao 44 katika michezo 131 ya michuano mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment