728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 10, 2016

    VODACOM KUMWAGA TUZO 13 LIGI KUU BARA,WAJUE WOTE WANAOZIWANIA,WACHEZAJI,MAKOCHA,MAREFA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    Hafla ya kukabidhi tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom
    Tanzania Bara kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Julai 17 mwaka huu.

    Jumla ya tuzo 13 za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa katika hafla hiyo
    itakayofanyika jijini Dar es Salaam, na kuratibiwa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

    Kamati hiyo inaundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka
    kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).

    Tuzo hizo ni mabingwa, makamu bingwa, mshindi wa tatu, mshindi wa nne, timu yenye nidhamu,mfungaji bora,mchezaji bora wa Ligi, kipa bora, kocha bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wa kigeni, goli bora la msimu na mwamuzi bora.

    Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba)

    Wakati kwa upande wa kipa bora ni Aishi Manula (Azam), Beno Kakolanya
    (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).

    Kocha bora wapo Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar)
    na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).

    Waliopendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi ni Farid Mussa
    (Azam), Mohamed Hussein (Simba),Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).

    Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba).

    Waamuzi bora katika kinyang'anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole
    Mwangole na Rajab Mrope.
    Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amewapongeza
    wateule wote waliopendekezwa kuwania
    tuzo hizo.

     "Kama wadhamini tuna
    matumaini makubwa kuwa msisimko wa ligi hii utazidi kuongezeka katika msimu
    ujao na kuzidi kuwapatia mashabiki wa soka wanaoifuatilia hapa nchini na nje ya nchi."

    Alisema Vodacom itaendelea kudhamini
    ligi hiyo kubwa ya soka nchini ili kutekeleza moja ya malengo yao ya kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji nchini. Pia kuwawezesha wachezaji kujipatia ajira na kuboresha
    maisha yao kupitia sekta ya michezo bila kusahau kuwapatia burudani wateja
    wake na Watanzania wote kwa ujumla.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VODACOM KUMWAGA TUZO 13 LIGI KUU BARA,WAJUE WOTE WANAOZIWANIA,WACHEZAJI,MAKOCHA,MAREFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top