728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 03, 2016

    KOCHA WA ZAMANI WA ASTON VILLA ATUPIWA VIRAGO ZAMALEK

    Cairo,Misri.

    Zamalek imemtimu kazi aliyekuwa kocha wake Mkuu Mscotland Alex McLeish baada ya kudumu naye kwa kipindi cha miezi mitatu pekee.

    Zamalek ilimuajiri McLeish mwezi Februari baada ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake wakati huo Ahmed Hossam ‘Mido kwa matumaini kwamba kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Aston Villa na Birmingham City angebadili hali ya mambo klabuni hapo lakini hali imekuwa kinyume badala yake miamba hiyo ya Cairo imendelea kusuasua katika michezo ya Ligi kuu ya Misri.

    McLeish ameiongoza Zamalek katika michezo 10 akifanikiwa kushinda michezo sita,akitoka sare mara mbili na kufungwa mara mbili huku mafanikio pekee yakiwa ni kuiwezesha Zamalek kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF.

     Zamalek inatarajia kumpa McLeish kitita cha dola ($)60,000 kama fidia ya kumfuta Kazi.McLeish nakuwa kocha wa nne kutimuliwa na Zamalek msimu huu baada ya Jesualdo Ferreira, Marcus Paqueta na Ahmed Hossam ‘Mido’.

    Wakati huohuo bodi ya Wakurugenzi wa Zamalek inayoongozwa na Rais wake Mortada Mansour inatarajiwa kumtangaza mrithi wa McLeish siku si nyingi lakini kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha wa muda Mohamed Helmy.

     

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA WA ZAMANI WA ASTON VILLA ATUPIWA VIRAGO ZAMALEK Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top