728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 03, 2016

    HUYU NDIYE MWAMUZI ALIYEBORONGA ZAIDI LIGI KUU ENGLAND.

    John Moss

    London,England.

    NI JOHN MOSS!!Utafiti umeonyesha kuwa Jon Moss ambaye alimlima kadi nyekundu yenye utata mshambuliaji wa Leceister City Jamie Vardy ndiye mwamuzi aliyefanya makosa mengi zaidi msimu huu kuliko waamuzi wote wanaochezesha ligi kuu nchini England.

    Utafiti uliofanywa na mtandao wa You Are The Ref.com umebaini kuwa msimu huu yamefanyika jumla ya makosa 84 katika jumla ya michezo 333 ya ligi kuu nchini England mpaka kufikia Aprili 22.

    Katika michezo 22 ya ligi kuu aliyochezesha mpaka sasa Moss amefanya makosa 13 yakiwa ni makosa sita zaidi ya Martin Atkinson,Roger East na Mike Jones yanaomfuatia.

    Mwamuzi aliyefanya makosa kidogo ametajwa kuwa ni Anthony
    Taylor.Taylor amefanya makosa matatu peke yake katika michezo 27 aliyochezesha hiyo ikiwa ni sawa na wastani wa makosa 0.11 kwa mchezo mmoja.

    KIGEZO KILICHOTUMIA KUBAINI MAKOSA!!

    Idadi hiyo ya makosa imetolewa kwa kuzingatia, bao kukubalia kimakosa au kukataliwa kimakosa,mchezaji kutolewa uwanjani kimakosa au kutotolewa uwanjani wakati alipaswa kutolewa.Penati kutolewa kimakosa au penati kutotolewa wakati ilipaswa kutolewa.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HUYU NDIYE MWAMUZI ALIYEBORONGA ZAIDI LIGI KUU ENGLAND. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top