728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 03, 2016

    HARRY KANE AJIA JUU CHELSEA,AIPA TANO LECEISTER CITY

    London,England.

    STRAIKA wa Tottenham Harry Kane ameishutumu Chelsea kwa kushangilia sare ya jana ya mabao 2-2 kama wao ndiyo waliotwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na siyo Leceister City.

    Akifanya mahojiano na BBC Kane,22 amesema "Kama mabingwa wa zamani wanashangilia sare namna ile tena kama wametwaa ubingwa,hii inaonyesha kuwa Tottenham tumefanya vizuri msimu huu.Tunapaswa kuendelea hivi,tuna kikosi kizuri,kocha mzuri na wafanyakazi wazuri."

    Wakati huohuo Kane ameipongeza Leicester City kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kusisitiza kuwa wamestahiri kwani wamefanya kazi kubwa ambayo kila mtu ameiona.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HARRY KANE AJIA JUU CHELSEA,AIPA TANO LECEISTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top